Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Joseph Aoun, Rais wa Lebanon, amesema kwamba kulengwa Dhahia kusini mwa Beirut leo na Israel, na kuingiliana kwa tukio hili na kumbukumbu ya Siku ya Uhuru, ni dalili nyingine kuwa Israel inapuuzia wito wa mara kwa mara wa kusimamisha uvamizi wake dhidi ya Lebanon, na inaendelea kukaidi utekelezaji wa maazimio ya kimataifa, pamoja na juhudi na mipango yote iliyowasilishwa ili kumaliza kuongezeka kwa mvutano na kurejesha uthabiti si kwa Lebanon tu bali kwa eneo lote.
Ameongeza kuwa: Lebanon, ambayo takribani mwaka mmoja uliopita hadi sasa imekuwa ikifuata masharti ya usitishaji vita na kusimamisha hatua za uhasama, na imekuwa ikiwasilisha mipango na jitihada mfululizo, inaiomba tena jumuiya ya kimataifa kuchukua wajibu wake na kuchukua hatua kwa uthabiti na ukakamavu kusimamisha uvamizi dhidi ya Lebanon na watu wake, ili kuzuia mvutano mpya wowote unaoweza kulirudisha tena eneo katika mgogoro, na kuzuia kumwagika kwa damu zaidi.
Maoni yako